📍Golden Tulip Airport Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema lengo la Serikali ni kuimarisha na kuweka mazingira mazuri wezeshi ya kibiashara katika uwekezaji hapa nchini.
Rais Dk.Mwinyi aliyasema hayo wakati akizindua Muongozo wa Uwekezaji na Mfumo wa Kieletroniki wa Uwekezaji (ZIPA) wenye madhumuni ya kurahisisha utoaji wa huduma kwa wawekezaji ikiwemo usajili na upatikanaji wa cheti cha uwekezaji wenye jina la"ZANZIBAR INVESTMENT ELECTRONIC WINDOW" (ZieW).
Dk.Mwinyi amesema kukuza uwekezaji ni moja ya malengo makuu ya Serikali na kuleta Maendeleo.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇