Dar es Salaam, leo
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amewahimiza Waislamu nchini kuwapeleka watoto wao madrasa wakajifunze imani na maadili ya dini yao ya Kiislam na kumjua Mwenyezi Mungu.
Pia amewaasa Waislamu kuzingatia mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) hususan kuhusu uchamungu na tabia njema.
Kinana ameyasema hayo leo Machi 25, 2023 wakati wa hafla ya mashindano ya Quraani tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Faraja Foundation ya jijini Dar es Salaam.
"Tunaagizwa na Quraani, pia tunaagizwa na Mtume wetu (Muhammad - SAW) kuwa kila Muislamu anapaswa kuzingatia mambo mawili la kwanza 'taqwa' (uchamungu) na la pili 'akhlaki' (tabia njema).
"Kwahiyo ukizingatia 'taqwa' ukazingatia na maadili mema hakuna namna utapotoka, itakuwa hakuna haja hata ya sisi kuwa na wasiwasi kwamba maadili mabaya yanaweza yakatupitia," amesema Kinana.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndg Abdulrahman Kinana akikabidhi Zawadi kwa Ndg. Abdulkarim
Bakari Auzi Mshindi wa kwanza Upande wa Juzuu Kumi Katika Mashindano
ya Saba ya Quran yaliyoandaliwa na Faraja Islamic Foundation
yaliyofanyika leo Machi 25 jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇