Na Lydia Lugakila, Kyerwa
Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera Ina magari 8 mabovu ambayo yamesimama kwa muda mrefu bila kutumika ambayo pia yamekuwa yakitumia gharama kubwa katika matengenezo.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya pili kwa mwaka 2022/2023 kilichofanyika Machi 17,2023 katika ukumbi wa Rweru Plaza Henerco Rushala kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema kamati ya Fedha na mipango tayari ilikaa katika kikao cha Desemba 6, 2022 na kupendekeza kuuzwa kwa magari hayo na kuondolewa kwenye mali za Halmashauri.
Rushala amesema kuwa ili kuondoa gharama kubwa za kuyahudumia magari hayo yaliyotumika kuanzia miaka ya 1993, 2003, 2010 na kuendelee hivyo haina budi kuuzwa.
Aidha baada ya taarifa hiyo kukifikia kikao hicho wajumbe wa baraza hilo wamekubaliana kwa pamoja kuuzwa kwa magari hayo 8.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Bahati Henerco amesema kuwa hata magari mengine ambayo yanafika kwenye hatua kama hizo yafuatiliwe ili kutoendelea kuharibu fedha za Serikali kwa matengenezo Makubwa.
Henerco amesema hakuna haja ya kuishi na magari mabovu yanayokuwa kikwazo kwa Wananchi kukosa huduma za jamii.
Mwenyekiti huyo amemuomba Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, kuangalia upya mifumo ya uendeshaji wa Magari hayo ikiwemo kusimamiwa ipasavyo.
Hata hivyo diwani wa kata ya Bugomora Batinoluho Henerico amemuomba Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kuwasisitiza Madreva wanaopewa magari hayo kuyatunza ili kuepuka kuharibika yakiwa mapya na kuchunguza zaidi kinachoharibu magari hayo.
.jpeg)


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇