Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
MKUU
wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ameamuru kuvunjwa kwa
baadhi ya Madarasa ya shule ya msingi Majogo katika Kijiji cha Litula
kata ya Marambo kutokana na uchakavu wa majengo ya shule hiyo ambayo
yanahatarisha maisha ya wanafunzi na walimu.
Akiwa
katika ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo "ulipo nipo
toa kero yako sema kweli sio majungu",mkuu wa wilaya huyo alifanikiwa
kufika katika shule ya msingi Majogo na kuikuta shule hiyo ikiwa katika
hali ya uchakavu mkubwa wa majengo ambayo yanahatarisha maisha ya
wanafunzi.
Moyo
alisema kuwa haiwezekani wanafunzi wakaendelea kusoma kwenye madarasa
ambayo yamejawa na nyufa kila kona hivyo madarasa hayo yabomorewe haraka
iwezekanavyo.
Alimtaka
mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kujenga upya madarasa
hayo ili wanafunzi wa Kijiji cha Majogo waendelee kupata elimu
inavyotakiwa kwa faida ya Taifa.
"Uchakavu
mkubwa wa miundombini,kuhatarisha maisha ya wanafunzi na walimu, siwezi
kukubali hali ya shule ya msingi Majogo waendelee kusoma katika shule
yenye majengo hatarishi"alisema Moyo
Moyo
pia alimuagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea
kumalizia ujenzi wa vyoo vya shule ya msingi Majogo ili kuwalinda
wanafunzi na walimu kiafya.
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi walisema jengo la shule litaua
wanafunzi,waomba libomolewe haraka haraka kwa kuwa wameshajenga jengo
jipya la vyumba vya madarasa lakini havijamalizika.
Akijibu
hoja hizo mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Injinia
Chionda Kawawa alisema kuwa wameshatenga kiasi cha shilingi millioni 6
kwa ajili ya ujenzi wa matundu mapya ya vyoo na wamelichukua suala la
kumalizia ujenzi wa vyoo ya shule ya msingi Majogo.
Kawawa
alisema kuwa suala la umaliziaji wa jengo la shule ya msingi Majogo
wamelichukua na watalifanyia kazi haraka sana ili kunusuru maisha ya
wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo wa kwanza kulia akitembelea shule ya msingi Majogo kujionea hali halisi ya Madarasa ya shule hiyo yalivyochakaa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇