LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 22, 2023

BALOZI WA URUSI ASEMA NCHI YAKE INATARAJIA KUIONGEZEA TANZANIA IDADI YA UFADHILI WA NAFASI ZA MASOMO KUTOKA 90 HADI 120

Dar es Salaam, leo
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Balozi Andrey Avetisyan, katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mbarouk ameipongeza Urusi kwa fursa za masomo zinazotolewa na nchi hiyo kwa watanzania na kuomba fursa zaidi za ushirikiano katika sekta za kilimo, madini, afya na uhandisi.

Naye Balozi wa Urusi Andrey Avetisyan amesema Serikali ya Urusi inategemea kuongeza idadi ya ufadhili wa nafasi za masomo kutoka idadi ya nafasi 90 hadi 120 ili kutoa nafadi zaidi kwa Watanzania kunufaika na fursa za elimu zinazopatikana nchini Urusi.

Urusi imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali hususan sekta za elimu, afya, utalii na utamaduni, mafuta na gesi, ulinzi na usalama, madini, kilimo na uhandisi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarou akizungumza na kBalozi wa Urusi nchini, Balozi Andrey Avetisyan katika Ofisi Ndogo ya Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam, leo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages