Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema kuwa Mwaka 2009 Population Coverage ya Huduma za Simu ilikuwa asilimia 45 na sasa imeongezeka hadi kufikia asilimia 96,Teknolojia ya 2G coverage yake ni 96%,3G ni 72%,4G ni 55% na Geographical Coverage ya 2G ni 69%; 3G ni 55% na 4G ni 36%.
Mashiba ametoa takwimu hizo leo Februari 13,2023 Jijini Dodoma, wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mfuko huo mbele ya waandishi wa habari.
Amesema kwa upande wa ujenzi wa minara vijijini Mtendaji huyo amesema UCSAF imeingia mikataba kufikisha huduma katika kata 1,242 zenye vijiji 3,654, Wakazi 15,130,250 ambapo Minara 1,087 yenye vijiji 3,378 na wakazi 13,320,750.
"Utekelezaji unaendelea katika Minara 155 yenye vijiji 276 na wakazi 1,809,500 kwa ruzuku iliyotolewa yaTZS bilioni 199 ikiwemo pia Mradi wa kimkakati wa Zanzibar, Minara 42, Shehia 38 ruzuku TZS bilioni 6.9,"amesema Mashiba.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇