LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 9, 2023

THAMANI YA NSSF IMEONGEZEKA IMEFIKIA TRILIONI 6.6



Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha J. Mshomba akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita katika mkutano na vyombo vya habari leo Februari 08, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa akiongoza mkutano huo.
Wanahabari wakiwa makini kufuatilia mkutano huo.










PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita, thamani ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imeongezeka na kufikia shilingi trilioni 6.6 mwezi Desemba 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 39 kutoka shilingi trilioni 4.7 iliyofikiwa mwezi Machi 2021


Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mshomba amesema pia  mapato ya uwekezaji 2022/23 yanatarajiwa kuendelea kuwa shilingi bilioni 700 kiasi ambacho ni ongezeko kubwa ukilinganisha na miaka ya hivi karibuni ambapo mapato hayo yalikuwa chini ya shilingi bilioni 500

Ametaja faida kwa mwaka 2022/23 inatarajiwa kuwa shilingi trilioni 1.27 ukilinganisha na faida ya shilingi trilioni 1.01 kwa mwaka 2021/22 


Ametaja mafanikio mengine kuwa ni kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mkulazi katika mwaka wa fedha 2022/23, Kiwanda hiki kinatarajia kupunguza changamoto ya uhaba wa sukari inayojitokeza mara kwa mara na kuilazimu Serikali kutegemea wazalishaji na waagizaji binafsi kuzalisha na kuagiza sukari kutoka nje


"Napongeza na kutambua mchango na ushirikiano tunaoupata kutoka kwa waajiri na wanachama wetu kote nchini kama sehemu ya mafanikio tuliyoyafikia hadi sasa na kuifanya NSSF kuwa moja ya mifuko mikubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati"


Ametoa atoa rai kwa baadhi ya waajiri wanaokiuka kanuni za uandikishaji wanachama na uwasilishaji michango ya watumishi walioko chini yao kuzingatia sheria za kazi na ajira na kutekeleza jukumu la kuwasilisha michango ya watumishi wao kwa mujibu wa sheria itakayowezesha ulipaji wa mafao kufanyika kwa wakati



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages