Na Victor Makinda. Igunga, Tabora
Kasi ya Serikali ya awamu ya sita ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hasssan, inaleta matumaini makubwa huku ikiibua furaha kwa viongozi na wananchi wa kada zote nchini.
Akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi Jimboni Igunga, Mbunge wa jimbo hilo, Nicholas Ngassa, alisema kuwa jimbo lake limepewa fedha nyingi za kuteleza miradi mikubwa ya maendeleo hali ambayo imeibua furaha kubwa na matumaini ya kuondokana na kero mbali mbali zilizokuwa zinawakabili wananchi.
Ngassa alisema kuwa miongoni mwa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayonedelea kutelekezwa jimboni humo ni miradi ya maji, afya, barabara, umeme na miradi ya elimu.
“ Serikali ya awamu ya sita, imelipatia jimbo la Igunga, Bilioni 21 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji katika vijiji 15 fedha zilizotokana na fedha za UVIKO – 19. Kwa upande wa miradi ya afya, Zahanati sita zimekarabatiwa na kujengwa vituo viwili vya afya vikubwa.” Alisema.
Aliongeza kusema kuwa Jumla ya shilingi 177 Milioni zimetolewa jimboni humo kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya kujifungulia Mama na Mtoto hospitali ya wilaya ya Igunga, sambamba na ujenzi wa jengo la huduma za wagonjwa mahututi (ICU).
Ngassa alisema kuwa jimbo la Igunga limefunguliwa kwa upande wa miundombinu kwani barabara zake nyingi zilikuwa hazipitiki hususani kipindi cha masika ambapo jumla ya shilingi 4 bilion zimepelekwa jimboni hapo kwa ajili ya ujenzi wa miundomini ya barabara ikiwemo madaraja makubwa mawili katika kata ya Mwamashiga na Kinungu.
“Ninaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongzo mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutekeleza Ilani ya CCM, kulipatia fedha nyingi za maendeleo jimbo la Igunga ambapo miradi mingi imekamilika kwa wakati na mingine inaendelea kutekelezwa hatua ambayo inawafanya wananchi wa jimbo hili kujawa na furaha na kuendelea kuiamini serikali na Chama Cha Mapinduzi.” Alisema Ngassa.
Katika hatua nyingine, Ngassa alisema kuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo jiimboni hapo unapaswa kwenda sambamba na uimarishwaji wa chama CCM kwa kuwa ndio chama dola ambacho kinatekeleza ilani.
“ Niliahidi kuwa nitajenga ofisi za chama kwa fedha zangu katika kata zote 16 jimboni Igunga na leo hii ninakuomba mwenyekiti wa CCM mkoa uzindue ujenzi wa ofisi hizo.” Alisema Ngassa.
Akizindua ujenzi wa ofisi hizo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora, Hassan Mwakasuvi, alimpongeza mbunge Ngassa kwa uamuzi wake wa kukiwezesha chama jimboni humo kufanya kazi kwa ufanisi huku akiwataka wananchi wa jimboni hilo kujitoa kwa hali na mali kusaidiana na mbunge huyo kufanikisha ujenzi wa ofisi hizo ambazo ujenzi wake unakadiriwa zitagharimu jumla ya shilingi Milioni 480.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇