LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 20, 2023

IGUWASAKUTUMIA BILIONI 1.8 KUJENGA MFUMO MAJI TAKA

 

Mkurungezi wa IGUWASA Hamphrey Mwiyombela , akizungmza na waandishi wa Habari Ofini kwake Juu ya mradi wa Mkubwa was ujenzi was mfumo was maji taka Mji wa Igunga.

NA ODACE RWIMO IGUNGA. 

MAMLAKA ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Igunga ( IGUWASA) wilayani Igunga Mkoani Tabora ipo katika hatua za mwisho kuanza ujenzi wa maji taka utakaogharimu bilioni 1.8. Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake mkurugenzi wa IGUWASA Humphrey Mwiyombela alisema ujenzi wa mfumo wa maji taka utasaidia kuongeza hali ya usafi katika mji wa Igunga ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira. 

Alisema mpaka hivi sasa wapo hatua za mwisho za kuanza kwa mradi huo mkubwa ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya mji wa Igunga kuwa wa kisasa zaidi kwani ujenzi huo utaenda sambamba na ununuzi wa magari mawili ya maji taka. 

Alisema kwa kipindi hiki hawana eneo rasmi ambalo hutumika kwa ajili ya kumwaga maji taka hali ambayo inaweza kusababisha hata milipoko ya mangojwa kwenye eneo ambalo hutumika kumwaga maji hayo. Katika hatua nyingine alizungumzia upatikanaji wa maji katika mji wa Igunga ambapo IGUWASA imefikia asilimia 89 ya kupeleka huduma kwa wananchi ikiwa ni kutaka kufikia malengo ya ilani ya Uchaguzi 2020-2025 ya upatikanaji wa maji kwa asilimia 95 ifikapo 2025. 

Alisema jambo kubwa wanaloendelea nalo ni kuhakikisha wanaongeza idadi kubwa ya watumia maji majumbani huku maeneo ya kata za zilizopo pembezoni mwa mji wakiendelea kubaini maeneo muhimu ya kuweka magati. Alisema kwa kuwa wilaya ya Igunga inakata moja tu iliyopo mjini hivyo kata nyingine zipo kijijini tunazozihudumia kama mamlaka ya maji tunaendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya maji safi kwa afya wa watu ili waweze kutuma maji safi na kuachana na maji ya madimbwi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages