Na, Lydia Lugakila Kagera.
MKUU wa Chuo Kikuu cha Dare es Salaam (UDSM), ambaye Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, amesema ujenzi wa chuo Kikuu Cha Dar es salaam tawi la Kagera unaotarajiwa kuanza mnamo Juni Mosi mwaka huu utatumia zaidi ya Shilingi Bilioni 18 huku chuo hicho kikitajwa kuwa mkombozi kwa Wana Kagera kiuchumi.
Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Ofisi za Mkoa wa Kagera kiilichowahusisha viongozi mbali mbali wa Mkoa huo Mkuu wa chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni 18 zitajenga chuo hicho hadi kukamilika kwake kwani tayari wametatua aina zote za vikwazo.
Amewahakikishiawananchi wa Mkoa huo kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Chuo hicho ni mkombozi kwao kwani fursa kubwa itaonekana hasa katika masuala ya kiuchumi ikiwemo kujifunza zaidi namna ya kuwekeza katika ufugaji wa Samaki pamoja na ujuzi mwingine unaoendana na walionao Mataifa Mengine.
Mhe, Kikwete Amesema hadi sasa wamefaikiwa kupata hati za ujenzi huku huo wakilenga zaidi kwa baadae chuo hicho kuitwa CHUO KIKUU CHA BUKOBA na kijitegemee kwa miaka ijayo.
"Chuo hiki kukamilika kwake kitaleta manufaa makubwa na kitakuwa na uhai mrefu kuliko Sisi wote, kitaendelea kuwepo na kitakuwa zaidi na kuwa manufaa kwa wana Kagera na Watanzania kwa ujumla "alisema Kikwete.
Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa UDSM, anayeshughulikia masuala ya taaluma, Prof, Bonaventure Rutinwa, amesema kuwa wazo la kuanzisha Chuo hicho ni wazo la Mkoa wa Kagera hivyo litumike zaidi hasa katika uwekezaji kiuchumi.
Aidha ameushukuru uongozi wa Mkoa huo kwa makubaliano ya upatikanaji wa eneo la ujenzi wa mradi huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila alisema uwepo wa chuo hicho ni ni mchango mkubwa sana katika kukuza uchumi wa Mkoa huo.
Hata hivyo Rc Chalamila amemuomba Rais huyo mstaafu wa awamu ya nne kuwa kozi zitakazotolewa katika Chuo hicho ziwasaidie katika kuakisi vivutio vilivyopo Mkoani humo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇