LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 9, 2023

WAZIRI NAPE: WEKENI USAWA UANDISHI WA HABARI ZA MIKUTANO YA HADHARA


 Waziri wa habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye amewashauri waandishi wa habari kuweka usawa katika uandishi wa habari za mikutano ya hadhara  ya kisiasa ikiwa ni siku chache baada ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kuruhusu mikutano hiyo kuanza kufanyika hapa nchini.

"Ni matumaini yangu kwamba waandishi wa habari mtaweka usawa wa stori zitakazotokana na mikutano hiyo kwa sababu tukibeba hivi hivi tunaweza kupeleka wananchi sehem mbaya  ambapo habari zingine zinakuwa na matusi uhuru uliotolewa utumike vizuri turekodi yale ambayo yatasaidisha nchi yetu,"  Amesema  Nape Nnauye.
Mheshimiwa Nnauye ameendelea kuwaasa waandishi wa habari kutumia weledi wao katika kuhakikisha wanaandika habari ambazo zitaleta manufaa kwa nchi na kwamba sio kila habari inaweza kupelekwa kwenye jamii kwani zingine hazina maana na zinaweza leta mgogoro katika nchi

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages