LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 14, 2023

WATU 4 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI MOROGORO




WATU wanne wa familia moja wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari dogo walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Kwambe Point A Dumila, wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Marwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ajali hiyo iliyotokea leo Januari 14,2023 ,saa mbili asubuhi maeneo ya Kwembe barabara kuu ya Dodoma- Morogoro ikihusisha gari dogo aina ya Spacial yenye namba T162DGM ikitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam iligongana na gari T654 DDN ikiwa na tela namba T418DDP ikitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Amewataja waliofariki ni Samil Ally ( 26) Mkazi wa Mbezi, Forstina Macha Paula Macha Mtumishi wa Kanisa, Rahma Said mtoto mwenye miaka 8 aliyekuwa anasoma darasa la nne na Sumay Said mtoto wa miezi 9 ,wote wakiwa wamehifadhiwa katika hospital ya St. Joseph iliyo Dumila wilayani Kilosa.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari dogo aina ya Spacial kutaka kulipita gari la mbele  na kugongana uso kwa uso na lori hilo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages