LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 7, 2023

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI JANUARI, 2023

 


CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mshambuliaji wa Barcelona na Uholanzi Memphis Depay, 28, anataka kujiunga tena na Manchester United miaka sita baada ya kuondoka Old Trafford. (Sport)

Manchester City wanapanga kuboresha safu yao ya kiungo msimu ujao kwa kumuongeza mchezaji wa kimataifa wa England anayekipiga Borussia Dortmund Jude Bellingham, 19 (ESPN)

Borussia Dortmund inatarajia uthibitisho wa Bellingham katika wiki zijazo kuhusu wapi anataka kucheza msimu ujao, huku Liverpool, Real Madrid na Manchester City zikisubiri kwa hamu uamuzi wake. (90Min)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Jude

Chelsea wanaendelea na mazungumzo na Shakhtar Donetsk kuhusu usajili wa winga wa Ukraine Mykhailo Mudryk, 22, na kiungo wa kati wa Benfica wa Argentina Enzo Fernandez, 21, baada ya kukamilisha dili la kumsajili kiungo Andrey Santos, 18, kutoka Vasco da Gama ya Brazil Ijumaa. (Metro)

Arsenal haitaki kujiingiza katika vita na Chelsea vya kutaka kumnunua Mudryk huku wakiongeza nguvu mipango yao ya kumsajili mshambuliaji wa Ureno Joao Felix kutoka Atletico Madrid. (Telegraph)

Kocha wa Gunners Mikel Arteta anashinikiza klabu hiyo kuwasajili Mudryk na Felix katika dirisha la usajili la Januari. (Mirror)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mudryk

Manchester United wamekubali kumsajili mshambuiaji wa Cameroon Vincent Aboubakar, 30, kwa mkopo kutoka Al Nassr. (OKAZ, via Talksport)

Juventus na Barcelona wanafuatilia kwa karibu hali inavyoenda ya kandarasi ya mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha katika klabu ya Crystal Palace, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anaingia katika miezi sita ya mwisho ya mkataba wake huko Selhurst Park. (Evening Standard)



CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Zaha

Liverpool na Chelsea wanaisaka saini ya kiungo wa kati wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21. (Sky Sports)

Chelsea pia wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Monchengladbach Mfaransa Marcus Thuram, 26 mwezi huu. (Foot Mercato)

Meneja wa West Ham David Moyes anakabiliwa na wiki mbili muhimu, huku mechi za Ligi kuu England dhidi ya Wolves na Everton zikipangwa kuamua mustakabali wake. (Mail)









No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages