LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 3, 2023

RAIS SAMIA: RUKSA VYAMA VYA SIASA KUFANYA MIKUTANO YA HADHARA, VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametangaza rasmi ruksa Vyama vya Siasa Nchini kufanya mikutano ya hadhara kuanzia  leo akisema mikutano hiyo ni haki ya kikatiba ya vyama hivyo.

Rais ametoa ruhusa katika kikao chake na Viongozi wakuu wa vyama vya siasa nchini kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jumanne, Januari 3, 2023.

“Moja ya jambo ambalo limezungumzwa sana hata kwenye kikosi kazi nilichounda kwa ajili ya kufuatilia hali ya kisiasa hapa nchini ni eneo la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Hivyo uwepo wangu leo mbele yenu nimekuja kutoa ruksa , lile tangazo la kuzuia mikutano ya hadhara sasa linaondoshwa.

Vyama vya siasa ni haki kuendesha siasa lakini upande wa Serikali tuna wajibu wetu nao ni kulinda mikutano hiyo ya hadhara ya vyama vya Siasa, na wajibu wa vyama vya siasa ni kufuata kanuni. nawaomba ndugu zangu, tunatoa ruksa hii, twendeni tufanye siasa za kistaarabu, siasa za kujenga nchi", alisema Rais Dk. Samia na kuongeza;

“CCM tuaamini kukoselewa na kukosoa, kosoeni, mimi naamini mkinikosoa najua changamoto iko hapa na changamoto niikifanyia kazi na kuitatua basi nitaendelea kuwepo. Ndio maana mimi siwaiti vyama vya upinzani bali ni vyama vinavyotuoneshe kasoro.

Rais akiwaomba vyama vya siasa kwenda kufanya siasa za kistaarabu, zenye kuheshimu mila na desturi alisema, ”Samia anaweza kuwa na uvumilivu, Samia anaweza kustahamili lakini chawa wa Samia anaweza asistahimili. Vyama vya siasa nendeni mkaseme waliahidi hawajatekeleza".

“Kazi yetu itakuwa ni kutekeleza. Twendeni tukafanye siasa, kama tumekosea haki za binadamu tuambieni, lakini tukitukanana, tukaanza kurusha makashfa nchi haitakalika. Nawaomba ndugu zangu twendeni tufanye siasa, isemeni Serikali na ikosoeni. Ukiamua kupanda jukwaani jizatiti na pale Serikali ambapo imefanya vizuri semeni.

Najua mtakwenda kusema Serikali ina madeni lakini semeni madeni yamefanya nini, yanajenga SGR hadi Kigoma. Uongo haujengi, bali jengeni hoja, nimekaa na kuzungumza na vyombo vya ulinzi na usalama na vitawalinda lakini tukumbuke hakuna ambaye yuko juu ya Sheria".

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wakuu wa Vyama vya Siasa nchini, kujadili masula ya kisiasa leo, Januari 3, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 
Baadhi ya Viongozi wakuu wa vyama vya Siasa wakimsikiliza Rais Dk. Samia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango akizungumza katika kikao hicho.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao hicho.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi akizungumza katika kikao. Kulia ni Rais Dk. Samia.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba wakati wa kikao hicho.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akisalimiana na baadhi ya Mawaziri wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Hashim  Rungwe katika kikao hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akiwa katika  picha ya kumbukumbu na Wenyeviti wa Vyama vya sisa mbalimbali nchini, baada ya kufanya kikao na viongozi hao leo Januari 3, 2023, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages