LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 11, 2023

PROF. MUHONGO KUITISHA KIKAO CHA KUTATHMINI MATOKEO YA MITIHANI MUSOMA VIJIJINI


Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 lina jumla ya Sekondari 27 ambazo:


*25 ni za Kata/Serikali

*2 ni za Madhehebu ya Dini (SDA & Katoliki)


Mbunge wa Jimbo ataitisha KIKAO cha kutathmini matokeo ya mitihani ya:


*Kidato cha Pili 

(Form II)

*Kidato cha Nne

(Form IV)


LENGO KUU

*Kutathmini matokeo ya mitihani ya vidato hivyo viwili kwa Wanafunzi wa Musoma Vijijini


*Kutoa mapendekezo ya kuboresha mbinu za kujifunza (uelewa) na kufundisha


Mahali pa kufanyika Kikao:

*Busambara Sekondari


Tarehe ya Kikao:

*Itategemea upatikanaji wa Matokeo ya Mitihani ya Form IV (2022).


Usafiri & Chakula:

*Mbunge wa Jimbo atagharamia




Miaka kadhaa ya nyuma, Mbunge huyo alishirikiana na Serikali ya Mkoa wa Mara kufadhili Kongamano la kuboresha Elimu Mkoani mwetu (Mara).


Walimu Wakuu (Headmasters) wa Sekondari zote 27, wanaombwa kujitayarisha.


Usisahau kutembelea Tovuti ya Jimbo letu ambayo ni:

www.musomavijijini.or.tz


Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

www.musomavijijini.or.tz


Tarehe:

Jumatano, 11.1.2023

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages