LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 20, 2023

PROF. MUHONGO AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA ELIMU BWAI SEKONDARI










Kata ya Kiriba ya Jimbo la Musoma Vijijini imepata Sekondari ya pili ili kutatua matatizo ya umbali mrefu unaotembewa na mwanafunzi wa Kata hiyo kwenda masomoni Kiriba Sekondari.

Vilevile, shule hiyo mpya, iitwayo Bwai Sekondari, itapunguza mirundikano ya wanafunzi kwenye madarasa ya Kiriba Sekondari.

BWAI SEKONDARI inajengwa na Kijiji kimoja cha Bwai Kumsoma.

Sekondari hii ilifunguliwa wiki iliyopita na hadi jana WANAFUNZI 125 kati ya 153 tayari wameanza masomo yao ya Kidato cha Kwanza (Form I) - 77.85% wameanza masomo.

HARAMBEE YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU

Jana, Alhamisi, 19.1.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliendesha HARAMBEE ya kuchangia ujenzi wa miundombini ifuatayo:

*Ukamilishaji wa vyumba 3 vya madarasa. Kwa sasa, vyumba vilivyokamilika na vinatumika ni vitatu (3)

*Ujenzi wa choo kipya chenye matundu manne (4). Kwa sasa, ipo choo yenye matundu nane (8)

*Ujenzi wa Jengo la Utawala ambalo msingi wake umekamilika. Kwa sasa, Ofisi ya Walimu ni chumba kimoja cha darasa.

Ujenzi ni endelevu, na michango ni endelevu hadi hapo miundombinu muhimu itakapokamilika, ikiwemo, maabara tatu (3) za masomo ya sayansi, maktaba, nyumba za walimu, viwanja vya michezo, n.k.

MICHANGO iliyopatikana:

Wanakijiji na Viongozi wao mbalimbali wakiongozwa na Madiwani wao 2 (Mhe Hamisi Saire & Mhe Bi Flora Magwa), na Viongozi wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa Kata, Ndugu Wanyanja Kabati walichangia:

*Saruji Mifuko 51
*Misumari kilo 3
*Fedha taslimu: Tsh 610,000
*Nguvukazi: wataendelea kujitolea kujenga bila malipo

Mbunge wa Jimbo amechangia:
*Saruji Mifuko 100
*Mabati bando 2 (mabati 24)

HARAMBEE YA UPATIKANAJI WA WALIMU WA KUJITOLEA

Bwai Sekondari ina jumla ya Walimu watano (5), akiwemo Mkuu wa Shule

Sekondari hii haina Walimu wa masomo ya:
English
Mathematics
Physics

Wanakijiji wakiwemo wazazi wa wanafunzi wanaosoma hapo, wameamua kuajiri walimu wa kujitolea kwa POSHO YA SHILINGI LAKI 2 kwa kila mwalimu kwa mwezi

*Wazazi watachangia Tsh 3,000 (elfu tatu) kila mwezi

*Mbunge wa Jimbo atachagia Tsh 100,000 (laki moja) kwa kila mwalimu kwa mwezi, yaani jumla ya Tsh 300,000 (laki tatu) kila mwezi kwa walimu watatu (3).

VITABU VYA MAKTABA

*Mbunge wa Jimbo ametoa box 4 za vitabu vya Maktaba kwa Sekondari hiyo mpya yenye kidato kimoja.

Picha za hapa zinaonesha matukio mbalimbali ya jana  kwenye shule mpya (Bwai Sekondari) ya Kijijini Bwai Kumsoma, Kata ya Kiriba.

KARIBUNI TUCHANGIE ELIMU KWENYE UJENZI WA BWAI SEKONDARI

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Ijumaa, 20.1.2023


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages