Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Msigani, Ubungo Jijini Dar es Salaam, Winfrida James Muhiji jana aliwaacha na tabasamu iliyojaa faraja Watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Yoco, baada ya kuwatembelea na kuwapatia mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula.
Katika safari ya kwenda kwenye kituo hicho, Mwenyekiti Winfrida alifuatana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Malamba Mawili Zawadi Mbwana, Katibu wa UWT Malamba Asili Tausi Habibu na Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Msigani Seif Kambangwa.
Wakiwa wenye hamasa ya kufanya tukio hilo, Mwenyekiti Winfrida na msafara wake, walibeba vitu mbalimbali ikiwemo mchele, maharage, mafuta ya kupikia na sabuni za kufulia na kuogea, hadi kwenye Kituo hicho eneo la Malamba mawili, watoto wakawapokea kwa furaha huku wakiimba nyimbo za kumtukuza Mungu kwa kupata ugeni huo.
Baada ya mapokezi, Kiongozi wa Watoto hao Fabian Simon alimweleza Mwenyekiti Winfrida wanavyoishi katika kituo hicho pamoja na changamoto zinazowakabili, ikiwemo shida ya upatikanaji wa vifaa mbalimbali vya shule na ada kwa kuwa wote wanasoma katika shule tofauti tangu za awali hadi sekondari.
Kabla ya kukabidhi vitu mbalimbali alivyofika navyo, Mwenyekiti Winfrida alisema, amejisikia kuwiwa juu ya watoto hao kwa kuwa anatambua kuwa wanaishi katika mazingira ya kutokuwa na Wazazi hivyo wanahitaji kupewa faraja ili wajisikie kama watoto wengine wanaoishi na Wazazi hasa katika nyakati za sikukuu kama za mwaka mpya, ndiyo maana akafika kwenye kituo hicho.
Alisema, pamoja na kufika kwenye kituo hicho kutmiza wajibu wake kama mwanajamii, lakini pia kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa UWT katika Kata ya Msigani, amefika kama njia ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuhakikisha Watanzania hasa watoto wanaoishi katika dhiki wanapata faraja.
"Watoto, kama mnavyojua Rais Samia anawapenda sana na amekuwa akifanya kila jitihada kuhakikisha watoto mnaoishi katika dhiki mnapata faraja, lakini kwa kuwa Nchi ni kubwa hawezi kufika kila mahala, hivyo sisi viongozi tunaoishi na ninyi ndiyo tunawajibu wa kumwakilisha kwa kufanya kama hivi nilivyofanya leo", akasema Winfrida.
Winfrida aliwaomba Watu wenye nafasi kusaidia Kituo cha watoto hao ili waweze kupata mahitaji muhimu ikiwemo vifaa vya shule, ada, vyakula na malazi.
"Nimeingia katika vyumba wanavyoishi watoto hawa, hali niliyoona nimeumia sana, mle vyumbani hakuna vitanda, wanalala chini kwenye magodoro, nawaomba wananchi kila mtu kwa nafasi yake ajitokeze ili tuwasaidie watoto hawa ambao ni nguvu kazi ya taifa la sasa na kesho", akasema Mwenyekiti Winfrida.
Mkurugenzi wa Kituo hicho Joseph Luzegama, ambaye ni mfugaji mchanga wa mifugo mbalimbali, alisema Kituo hicho hadi sasa hakina mfadhili lakini ni mtu mmoja mmoja ambao hutoa sadaka ya vyakula, ada na mahitaji mengine ya watoto.
Alisema Kituo hicho hadi sasa kina jumla ya watoto 28, 20 wakiume na wanane wasichana na kwamba watoto hao ni wenye umri wa miaka kuanzia minne hadi 20, ambao wote amewakusanya kutoka katika Vituo mbalimbali vya Ustawi wa Jamii.
"Kabla sijaanza kulea watoto hawa, nilianza kujitolea kusaidia wajane na watu mbalimbali wenye shida, na hadi sasa naendelea kusaidia wajane na watu mbalimbali wenye shida, lakini Agosti 4, 2017 ndiyo nilianzisha kuendesha rasmi kituo hiki", akasema Luzegama.
Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Msigani Seif Kambangwa, akiwa amebeba kiroba cha mchele msafara wa Mwenyekiti Winfrida ulipofika kwenye kituo hicho.
Watoto wa Kituo cha Yoco wakiwa wamewapokea wageni vizigo waliyofika nayo kwenye kituo hicho.
Watoto wa Kituo cha Yoco wakiwa wamepokea mizigo ya vitu mbalimbali vilivyoletwa na Mwenyekiti Winfrida kwenye kituo hicho.
Kabiti kanakolelewa kwenye Kituo cha Watoto yatima kakiwa amebeba kiroba cha mchele kwa furaha.
Mwenyekiti wa UTW Kata ya Msigani akiingia eneo la tukio baada ya kuwasili na ujumbe wake kwenye kituo hicho.
Mwenyekiti Winfrida na ujumbe wake wakishiriki kuimba wimbo wa kumtukuza Mungu uliokuwa ukiimbwa na watoto wa kituo hicho kupokea ugeni.
Kisha Mwenyekiti Winfrida na Ujumbe wake wakashiriki sala fupi iliyoendeshwa na watoto hao kukaribisha ugeni.
Mtoto wa Kituo hicho Ezeku Ernest akiongoza mamombi ya kuwabariki Mwenyekiti Winfrida na ugeni wake,
Mtoto Ernest wa kituo hicho akiendelea kuongoza mamombi ya kuwabariki Mwenyekiti Winfrida na ugeni wake.Mwenyekiti Winfrida akizungumza na watoto wa Kituo hicho.
Mwenyekiti Winfrida akiendelea kuzungumza na watoto hao kwa upendo mkubwa.Kiongozi wa watoto hao akipokea zaadi kwa furaka kutoka kwa Mwenyekiti Winfrida.
Kiongozi wa watoto hao akiendelea kupoea zawadi mbalimbali kwa naiaba ya watoto wenzake.
Kisha watoto wakafanya maombi ya shukurani kwa zawadi walizopokea.
Kisha Mwenyekiti Winfrida na ujumbe wake wakapigwa picha na kumbukumbu na watoto wa kituo hicho.
Mwenyekiti Winfrida akizungumza na Mkurugenzi wa Kituo hicho kabla ya kuondoka.
Mwenyekiti Winfrida akienda kuona wanakolala watoto wa Kituo hicho.
Mahala wanakolala watoto wa Kituo hicho👆, ambako baada ya Mwenyekiti Winfrida kupaona alisikitika na kuomba watu mbalimbali kusaidia ili watoto hao walale katika mazingira mazuri.👇
Mwenyekiti Winfrida akitazama kwa huzuni wanapolala watoto wa Kituo hicho.
Kisha akatoka na ujumbe wake.
Mkurgenzi wa Kituo hicho akiwaongoza kutoka, Mwenyekiti Winfrida na Ujumbe wake, baada ya kuona wanapolala watoto. ENDS
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇