WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ,akizungumza wakati akizindua bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma.
Mkenda amesema kuwa bodi hiyo ina kazi kuu mbili ambazo ni uwezeshaji na udhibiti ili kuboresha elimu nchini.
Aidha ameitaka bodi hiyo kusimamia vyema ajira ya wakufunzi wa vyuo vikuu ili kuwapata wenye uwezo unaostahili kufundisha katika vyuo hivyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof.Penina Mlama,akitoa taarifa wakati wa uzinduzi wa bodi ya Tume hiyo hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma.
Prof. Mkenda akiwakabidhi zana za kufanyia kazi baadhi ya wajumbe wa tume hiyo.
PROF. Mkenda akiwa na baadhi wa wajumbe wa bodi hiyo
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Waziri Mkenda akitoa maagizo hayo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇