LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 19, 2023

MAKAMU WA RAIS GAMBIA AFARIKI DUNIA

 Makamu wa Rais wa Gambia Badara Alieu Joof amefariki dunia nchini India.


Rais wa nchi hiyo Adama Barrow ametangaza kuwa Makamu huyo wa rais amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, ingawa rais hakutaja iwapo alikuwa akipokea matibabu nchini India au la.


Rais Adama Barrow alimteua Joof kama makamu wa rais baada ya kushinda uchaguzi wa marudio mnamo Disemba 2021.


Makamu wa rais aliwahi kuwa waziri wa elimu zamani.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages