SHIRIKISHO la Machinga (SHIUMA) Mkoa wa Pwani limemtakia heri ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan (pichani) ambaye leo ni kumbukumbu ya siku yake za kuzaliwa.
"Kwa huruma yako unayoinyesha kwetu machinga hatuna budi nasi kukuonyesha kwamba nasi tuko nawe," alisema Filemon Igans Maliga, Mwenyekiti wa SHIUMA Mkoa wa Pwani akiungwa mkono na Katibu wa shirikisho hilo Pwani, Godfrey Lukas.
Akifafanua zaidi Lukas alisema Rais amekuwa msaada mkubwa kwa machinga na hata ahadi zake kwa machinga amekuwa ni mwenye kuzitekeleza kwa hali ya juu.
Katika matangazo yaliyoandaliwa na kusambazwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mafunzo wa SHIUMA, Dismas Lyassa, wakuu hao wa SHIUMA walionyesha kufurahishwa na mchango wa Rais Samia katika kusaidia machinga na maendeleo kwa ujumla nchini.
"Anazifahamu changamoto za machinga na amekuwa akichukua hatua kuzitatua, kwa mfano aliahidi machinga tuwe na ofisi, tayari jitihada zinaendelea kupitia ofisi ya Mkuu wetu wa Mkoa wa Pwani, tayari tumepata eneo na mipango mingine ya ujenzi inaendelea," aliongeza Maliga.
Viongozi hao pia wamepongeza ushirikiano mzuri wanaopata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge katika shughuli zao za umachinga na mkakati wa ujenzi wa ofisi ya machinga katika mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇