Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega Heneriko Kanoga akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo kwenye kikoa maalumu cha bajeti. |
Ametoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya madiwani kuonekana kutoridhishwa na mwenendo wa ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye vyanzo vilivyoainshwa kwenye bajeti ya 2021/2022 kuelekea bajeti mpya ya 2023/2024.
Alisema kuna sehemu ambayo hawaendi sawa kwani ukiangalia kwenye vyanzo vingi ambayo ndivyo tegemewa kupata mapato ukusanyaji wake hauendani na uhalisia wa vyanzo hivyo ambapo kunaoneka uzembe mkubwa wa utendaji kazi.
“ Ukiangalia kilichoandikwa hapa kwa mfano gulio lilopo kata ya Ubinga tunaelezwa mapato kwa wiki ni shilingi 35000 lakini tulisha tuma wajumbe wa kamati ya fedha kukusanya mapato eneo hilo ambapo kwa wiki walipata zaidi ya laki 500,000 je huu ni uzembe au tuite udanganyifu”alihoji Kanoga
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega wakiwa kwenye kikao maalumu cha bajeti ya 2023/2024 |
Napenda kukuagiza mkurugenzi angalia vizuri huu ukusanyaji mapato kwa watu wako kuna uzembe mkubwa ikiwezekana anza kuchukuwa hatua za kinidhamu kwa mtu yeyote ambaye anataka kutukwamishwa kutotimiza malengo yetu.
Kwa upnde wake diwani wa kata ya Isagenhe Salumu Kabadi alionesha kutolidhishwa na kasi ya ukusanyaji mapato kwa watendaji waliopewa dhamana kwani watu wameshindwa kufikia malengo ya bajeti iliyopitishwa na baraza la madiwani kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Alisema ili kuweza kufikia malengo ya halmashauri kunaulazima wa kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo mbalimbali ambavyo vipo kwenye mpango wa bajeti bila uwepo wa udanganyifu kwa wakusanyaji waliopewa dhamana ya kufanya kazi hiyo.
Naye diwani wa kata ya Uduka Majonas Mshingo alisema mwenyekiti anatakiwa kuwa mkali hasa kwenye suala la ukusanyaji wa mapato ili halmashauri hiyo iweze kuwa hata ya kwanza kitaifa kwenye ukusanya wa mapato ya ndani.
Alisema halmashauri hiyo inavyanzo vingi vya kujipatia mapato kwani huwezi kusema halmashauri haina hela wakati wanakata zaidi ya 30 ambazo zote zina minada na magulio mengi ambayo yanaweza kutoa mapato mengi sana.
Hata hivyo kwa upande wa kaimu mkurugenzi halmashauri ya Nzega Mohamed Omary alisema kwa sasa watazingatia mahitaji ya bajeti iliyopitishwa na baraza la madiwani.
Alisema bajeti ya mwaka 2023/2024 imezingatia mahitaji maalumu ya halamashauri hiyo kwa asilimia kubwa huku mapato ya ndani yakipewa kipaumbele hasa katika miradi mbalimbali itakayotekelezwa.
Alisema bajeti ya mwaka 2023/2024 halmashauri ya wilaya ya Nzega inakadilia kukusanya na kutumia bilioni 44.463 ambapo kati ya hizo bilioni 2.167 ni kutokana na mapato ya ndani na upande wa ruzuku kutoka serikali kuu ni bilioni 26.862 kati ya hizo billion 25.151ni mishahala ya watumishi.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇