Mmoja wa wazazi waliojifungua siku hiyo ya mkesha wa Chrismas
muuguzi kiongozi idara ya afya ya uzazi na kizazi bi Grory Kagaruki
Na Lydia Lugakila,
Bukoba.
Jumla ya watoto 5 wamezaliwa mkesha wa siku kuu ya Krismas katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera huku akina mama waliojifungua katika mkesha huo, wakimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uboresha ya miundo mbinu ya hospitali hiyo ikilinganisha na mwaka 2018.
Wakizungumza na mtandao huu akina mama hao wakiwa bado wanaendelea kupata huduma katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera akiwemo Bi Monica John aliyefanikiwa kupata mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji amempongeza Rais Do
kta Samia kwa namna alivyoweza kuboresha majengo na vifaa tiba.
"Namshukuru Mungu kwa kupata mtoto huyu wa kiume katika siku hii kubwa na muhimu, zaidi na zaidi nimshukuru Rais Dokta Samia kwa kuboresha miundombinu kwani nakumbuka mwaka 2018 wakati nakuja hapa kujifungua jengo la akina mama wanaojifungua lilikuwa ni bovu muda huu limepanuka hata vitanda vimeongezeka miaka ya nyuma kitanda kimoja kulikuwa na uwezekano wa kulala watu akina mama wawili" alisema Bi Monica.
Ameongeza kuwa wamefanikiwa kupata huduma bora ya kimatibabu pamoja na watoto wao huku akimuomba Rais Samia kuendelea kuongeza bajeti na motisha kwa wahudumu wa afya ili kuwawezesha kuendelea kutoa huduma bora.
Naye Bi Leticia Samweli aliyepata mtoto wa kike amepongeza namna alivyopta huduma bora kutoka kwa wahudumu wa hospitali hiyo na kuiomba serikali kuwapambania wahudumu hao ili wawe kuwa na moyo katika utoaji huduma.
Kwa upande wake muuguzi kiongozi idara ya afya ya uzazi na kizazi bi Grory Kagaruki kwa niaba ya uongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera amesema kuwa watoto 5 wamezaliwa wakiwa hai ambapo wanne ni wa kiume mmoja wa kike na kuwa waliojifungua kwa njia ya upasuaji ni wawili.
Aidha Bi Kagaruki ametumia nafasi hiyo kuwaomba akina mama wajawazito kujitahidi kuwahi kliniki tu mara wanapohisi kuwa ni wajawazito ikiwa ni pamoja na kuudhuria kliniki kama wanavyokuwa wamepangiwa na mtoa huduma.
Hata hivyo amewakumbusha kuudhuria baada ya kujifungua ili kuweza kuendelea kuhakiki kama kuna dalili za hatari huku akiitaja changamoto ya baadhi ya kina mama wajawazito kufika katika vituo vya afya wakiwa katika uchungu na kusababisha kuwepo kwa tatizo la akina mama kuwa na tatizo mkubwa la upungufu mkubwa wa damu, mtoto kufariki akiwa tumboni na mtoto kuzaliwa kabla ya wakati.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇