LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 30, 2022

RONALDO KUONGOZA KUTOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUMUAGA PELE

 'Asante, Mfalme': Brazil yatoa heshima kwa Pele

  1. m

    Brazil imeanza siku ya kwanza bila gwiji wa soka Pele.

    "Mfalme", ambaye alishinda Kombe la Dunia mara tatu na alikuwa mwanasoka bora zaidi wa wakati wote, amefariki akiwa na umri wa miaka 82 huko Sao Paulo siku ya Alhamisi.

    Usiku kucha, picha ya uso wa Pele uling'aa kwenye majengo katika taifa zima la Brazil na alama ziliwashwa taa katika kumbukumbu yake.

    Mashabiki waliingia barabarani wakiwa wamevaa tshirt lake la kipekee la nambari 10.

    Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

    mm

    Mashabiki walianza kukusanyika nje ya hospitali ya Albert Einstein ya Sao Paulo siku ya Alhamisi mchana waliposikia habari za kifo cha Pele.

    Bendera iliandikwa "Mfalme wa Milele Pele". Pele alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo tangu mwaka 2021.

    Wakati hali yake ilipozidi kuwa mbaya, Wabrazil walikuwa wametumia wiki kadhaa kutafakari maisha yake na historia yake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages