Baadhi ya viongozi wa dini wakimsikiliza mkuu wa mkoa
Na Lydia Lugakila Kagera.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyouwezesha mkoa huo kuwa na miradi mingi ya kimaendeleo.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri mkoa (RCC) kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kilicholenga kujadili ajenda mbalimbali za maendeleo ya mkoa na utekelezaji wa majukumu ya serikali mkuu wa mkoa wa Kagera Albet Chalamila amesema kwa jitihada za Rais Dkt Samia zimeupa nguvu mkoa huo katika kuendelea kuonekana wa tofauti katika miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na namna anavyoiongoza nchi.
Amesema kuwa Rais Samia amefanya makubwa katika Mkoa wa Kagera ikiwa ni pamoja na kuelekeza miradi mingi ya maendeleo ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shilingi Bilioni 79.5 zimetumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Fedha hizo ni nyingi na zinahitaji usimamizi mkubwa hivyo naahidi kuwa tutaendelea kusimamia fedha hizo kwa nidhamu ya juu kwa maslahi ya mkoa na taifa kwa ujumla" alisema Rc Chalamila.
Aidha amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023 hadi septemba 2022( robo ya kwanza ) tayari mkoa wa Kagera umekwisha pokea shilingi bilioni 21.0 ambapo kati ya fedha hizo nyingi zilikuwa ni kwa ajili ya sekta ya elimu, Afya, pamoja na sekta mbali mbali.
Ameongeza kuwa katika suala la elimu Rais Samia amewaunga mkono kwani kwa awamu ya kwanza mkoa huo ulipokea Bilioni 17 na milioni 620 kwa ajili ya kutengeneza vyumba vya madarasa 881 na kwa awamu ya pili Bilioni 10 milioni 280 zimetumika kwa ajili ya kujeng madarasa 514 ili kukabiliana na uhaba wa madarasa kwa mwaka 2023.
Amesema ujenzi huo wa madarasa umefikia asilimia 85 pamoja viti ambapo kufikia mwezi Januari 2023 wanafunzi wote waliochaguliwa na wanoingia darasa la kwanza watakuwa wameripoti vizuri bila kikwazo.
"Dhana ya elimu bila malipo kwa mwaka wa fedha 2012/ 2022 mkoa pia ulipokea shilingi bilioni 16.5 kwa ajili ya ada madarasa kwa wakuu wa shule na waratibu elimu kata," alisema Chalamila.
Hata hivyo amesema kufikia robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023 mkoa huo pia umekwisha pokea Bilioni 4.8. huku akisisitiza zaidi utunzaji wa miradi hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇