LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 26, 2022

KINARA WA MASOMO SHULE YA FEZA APONGEZWA

 





 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Afya, Grace Maghembe amemkabidhi cheti na kumpongeza mwanafunzi bora kwenye masomo Kidato cha Nne Shule ya Wavulana Feza, Brian Nick Juma kwenye mahafali yaliyofanyika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam


Grace Maghembe akipongeza kijana huyu kwa juhudi kubwa alizofanya toka anasoma na kufanya vyema kipindi chote cha cha elimu yake ya kidato cha nne akiongoza darasani katika Shule za Feza pia aliwaomba wazazi kwa ujumla kuwa karibu na watoto wao kipindi cha masomo hili kuwajengea uwezo mzuri vijana wao 

Pia mzazi wa kijana huyo, Brian  Nick Juma alishukuru uongozi wa shule hiyo kwa juhudi kubwa ya kuwajenga watoto wao kielimu na kuwa na uwezo mkubwa wa kimasomo darasani na hata wao hawakutarajia mtoto wao atakuwa bora kiasi hicho.

 Aliendelea kuwasihii wazazi wote walio shiriki mahafali hayo, kuwafuatilia watoto wao kwa ukaribu sana kwenye masomo yao kwani kunawajengea umakini na uwelewa tosha kwenye masomo na kuja kufanya vizuri darasani.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages