LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 25, 2022

DK. MPANGO: WATANZANIA TUOMBE TOBA KWA MUNGU KUFUTA MATENDO YA UKATILI YANAYOKITHIRI DHIDI YA WATOTO

Dodoma, leo
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, ametoa mwito kwa Watanzania kuomba toba kwa Mungu kwa matendo ya kikatili kwa Watoto na kuacha dhuluma dhidi yao, huku akiwasihi kutimiza mahitaji ya watoto katika kuwatunza ikiwemo kuhakikisha wanapata elimu.

Akizungumza leo baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Krismasi katika Parokia ya Kristo Mfalme, Veyula mkoani Dodoma, pia ametoa mwito kwa Watanzania kuongeza jitihada katika kuimarisha ulinzi wa watoto ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyowakumba.
 
Kuhusu mvua zilizoanza kunyesha hapa nchini, Makamu wa Rais pia ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya uwepo wa mvua hizo katika kuzalisha mazao na kupanda miti ili kuhifadhi mazingira.

Amesema ni muhimu suala la upandaji miti kuanza katika ngazi ya familia kwa kupanda miti mitatu kila familia na hivyo kupendezesha nchi na kulinda mazingira.
 
Katika ibada hiyo, Makamu wa Rais ameambatana na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango na ibada imeongozwa na Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme iliyopo Veyula Dodoma Padre Saimon Katembo.

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, akizungumza leo baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Krismasi katika Parokia ya Kristo Mfalme, Veyula mkoani Dodoma. Kushoto kwake ni Mama Mbonimpaye Mpango.
Waumini wakiwa kwenye Ibada hiyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages