LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 2, 2022

DC MPOGOLO ASHIRIKI KAMPENI YA KITAIFA CHANJO YA POLIO SAME





 Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogolo ameshiriki kikamilifu zoezi la kampeni ya kitaifa ya chanjo ya polio awamu ya nne katika hospital ya wilaya ya Same kilimanjaro.


Wakati akimpatia mmoja wa watoto chini ya umri wa miaka mitano  chanjo hiyo amewataka wazazi wenye watoto walio na umri chini ya miaka mitano wajitokeze hili watoto wao wapate chanjo hiyo na kuwakinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kupooza (polio)

DC Mpogolo aliendelea kusisitiza kwa watoa huduma ya Afya ya chanjo ya polio kutoa Elimu kwa kila kaya juu ya mlipuko wa ugonjwa wa kupooza (polio) lengo ni kuwalinda watoto wote wawe salama maana ni taifa la kesho.

Kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Same Doctor Alex amesema timu ya wataharamu ambayo wanatoa huduma ya Afya ya chanjo ya polio imesambaa karibu vijiji vyote kutoa Elimu juu ya mlipuko wa ugonjwa wa kupooza (polio) huku wakiakikisha mtoto chini ya umri wa miaka mitano anapata chanjo hiyo 

Mratibu wa chanjo wilaya ya Same Mr Pilula  amesema hospital ya wilaya ya Same imejipanga kikamirifu kuakikisha zoezi hili la utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano linakamilika na kuakikisha kila mtoto anapata chanjo hiyo.

Mmoja wa wazazi ameshukuru kwa juhudi kubwa za viongozi wa wilaya ya Same pamoja na watoa huduma wa chanjo ya polio. kuwa kazi wanayoifanya kuakikisha watoto wao wapo  salama, na kuwataka wazazi wengine wasiwafiche watoto na kuwa na imani potofu juu ya chanjo hiyo inayotolewa nchi nzima

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages