LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 31, 2022

CHANG'OMBE LADIES WALIPOFANYA TUKIO LA KUFUNGA MWAKA 2022, WAMUIBUA BABA MZAZI WA MWANAHABARI NGULI TIDO MHANDO

CCM Blog, Temeke
Kinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chang'ombe, Temeke Jijini Dar es Salaam (Chang'ombe Ladies) juzi walianya tukio la funga mwaka wa 2022, kwa kutembelea wazazi wodini na wazee nyumba kwa nyumba hadi kumuibua Baba Mzazi wa  Mwanahabari nguli Tanzania na Duniani kwa jumla Dunstan Tido Mhando.

Kabla ya kumuibua Mzee Prof. Mhado mwenye umri wa miaka 98 (2022), Wanawake hao wakiongozwa na Mbunge wa Temeke Dorothy Kilave kwanza walipiga shoto-kulia wakiwa wamevalia sare zao hadi Kituo cha Afya Yombo Vituka na baada ya kupokewa wakaingia katika wodi ya Wazazi na kuwapa faraja kwa bashasha na tabasam huku wakiwagawia vitu mbalimbali vikiwemo taulo za kike, sabauni za kuogea na za kufulia.

"Hongereni sana, kina mama wenzetu, leo tumekuja kuwatembelea ili kuwajulia hali na pia tugawane tabasamu maana hapa mlipo ni mahala magumu, mnahitaji kupewa faraja. pia kama mnavyojua 'mkono mtupu haulambwi', hivyo tumewaletea na zawadi kidogo. tunajua havitakidhi haja zenu lakini tumeleta kwa ajili ya kuonyesha upendo tu", akasema Mbunge Kilave kwa nyakati tofauti wakati kina mama hao wakisalimia hapa na pale na kugawa zawadi.

Pamoja na Mbunge huyo, pia Mwenyekiti wa Umoja wa Kinamama hao Dada Angela na Katibu wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mstaafu Angelina Akilimali walikuwepo katika tukio hilo.

Baada ya kutoka Kituo hicho cha Afya ndipo wakaanza safari ya kwenda kusalimia Wazee, ambapo waliwatembelea kinamama Wazee na Prof. Mzee Mhando. Mzee Mhando licha ya kuwa na umri mkubwa wa miaka 98 lakini aliweza kuonyesha kuwa bado yupo imara katika mambo mengi ikiwemo kutunza kumbukumbu kichwani.

Habari Picha👇

Mwenyekiti wa Kikundi cha Kinamama  cha Chang'ombe Ladies Angela Bondo (Wanne kulia) akikabidhi rasmi zawadi mbalimbali kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Yombo Vituka Dk. Boniface Mduma, wakati Kinamama hao walipotembelea Kituo hicho cha Afya kwa ajili ya kuwapa furaha kinamama wazazi na kuwagawia zawadi hizo, ikiwa ni sehemu ya kuuaga mwaka 2022, juzi. Kulia ni Katibu wa Kikundi hicho Angel Akilimali na Watatu kulia ni Mbunge wa Temeke Dorothy Kilave. m

Zifuatazo ni mfululizo wa matukio hatua kwa hatua ya ziara hiyo👇 Baadhi ya Kinamama wa Kikundi hicho wakiwa na zawadi walipowasili kwenye Kituo hicho cha Afya. Mwenyekiti wa Kikundi cha Kinamama  cha Chang'ombe Ladies Angela Bondo akikabidhi rasmi zawadi hizo kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Yombo Vituka Dk. Boniface Mduma. Kulia ni Katibu wa Kikundi hicho Angel Akilimali na Watatu kulia ni Mbunge wa Temeke Dorothy Kilave. Ujumbe wa Kinamama hao ukiongozwa na Dk. Mduma kwenda Wodi ya Wazazi kuwasalimia waliojifungua na kuwagawia zawadi. Kushoto ni Mlinzi wa Kituo hicho cha afya akisaidia kubeba zawadi. Mbunge Kilave na Kina Angel wakisubiri kuingia Wodi ya Wazazi. Mbunge Kilave akijitambulisha yeye na Ujumbe wa Kinamama wenzake baada ya kuingia katika Wodi ya Wazazi kwa ruhusa maalum ya Daktari. Mbunge Kilave akimpatia zawadi mama aliyejifungua mtoto katika Wodi hiyo. "Hebu tuone katoto kako, lohh kazuri sana, Hongera", akasema Mbunge Kilave wakati akimbeba mtoto wa Mama huyo. "Nimekapenda kape jina langu", akasema Mbunge Kilave."Haya Mama na wewe zawadi yako hii. Hongera sana", akasema Mbunge Kilave kwa Mama huyu.Katibu Angel Akilimali akimpatia zawadi kwa bashasha mama aliyejifungua katika wodi hiyo ya Wazazi. Katibu Angel akitoa zawadi kwa Mama aliyejifungua mtoto katika Wodi hiyo. Kisha Katibu Angel akabeba Kachanga kwa furaha. Mwenyekiti Angel nayeye akaburudika kubeba kachanga ka Mama huyu (kulia). "Mwaya, unakaonaje katoto haka, kazuri sana", Mwenyekiti Angel akasema kumwambia Wajina wake Katibu Angel (kushoto). "Hongera sana Mama, umejifungua mtoto huyu ukiwa na umri wa miaka 19 tu! Hongera mno", akasema Mwenyekiti Angel wakati akiwa amebeba kichanga cha mama huyo (katikati), Kulia ni Mbunge Kilave naye akifurahia.Katibu wa Mbuge Kilave ambaye pia alikuwepo, akapata nafasi ya kufurahia kichanga cha mama huyu (kulia). mMbunge Kilave akipigwa picha ya kumbukumbu na wauguzi katika Wodi hiyo ya Wazazi. Kulia ni  Dk, Mduma. "Kwa wazazi tumemaliza sasa kama zawadi zimebaki kuna wajawazito wapo kulee, ikiwapendeza twendeni nao mkawapatie", akasema Dk. Mduma. Mbunge Kilave na wenzake wakaanza kushoto-kulia kwenda kwa wajawazito waliko.  

Baada ya kufika kwa wajawazito wanaosubiri huduma👇"Jamani kati yenu nani anamjua huyu, hata kwa cheo chake tu?" Dk. Mduma akawauliza Kinamama wajawazito, wakajibu wote, wakisema "Huyo ni Mbunge wa Temeke Mama Kilave". Mbunge Kilave na Dk. Mduma wakaanza kuwapatia zawadi. "Haya zawadi yako hii", akasema Mbunge Kilave wakati akimpa zawadi ya taulo ya kike mmoja wa Wajawazito hao.Mwenyekiti Angel na Mbunge Kilave akitoka baada ya Kikundi cha Kinamama hao kugawa zawadi kwa wajawazito. Katibu Angel akizungumzia tukio lote na Mtangazaji wa Chanel ten. Kushoto ni Mwenyekiti Angel. 

Kisha wakaondoka kwenye Kituo hicho cha Afya kwenda sasa kwa wazee 👇

=====

Wakaingia nyumbani kwa Bibi Mama Kazimili, ikawa ni stori na kicheo mwanzo mwisho👇"Haya kwa herini Wanangu, Karibuni tena". akasema Mama Kazimili. Ikafuatia safari ya kwenda kwa Prof. Mhando👇 Wakiingia getini.

Wakalakiwa na mtoto wa Prof Mhando.
Prof. Mhando akawasili sebuleni huku wageni wake wakimshangilia.
"Karibuni sana wanangu na wajukuu zangu", akasema Pfro Mhando kuwakaribisha kinamama hao.
Mwenyekiti Angel (watatu kulia), akitambulisha ugeni aliofika nao. Kushoto ni Prof Mzee Mhando akisikiliza kwa makini utambulisho huo.
Baada ya stori za hapa na pale kama ilivyo kwa Babu na wajukuu, wakamkabidhi zawadi.

Mbunge Kilave akasimama kumshukuru Prof Mzee Mhando.
Kisha Prof Mzee Mhando akafanya sala ya shukurani kabla ya ugeni kuondoka. 

Halafu ikafuatia safari ya kweneda nyumbani kwa Bi Lilian Bridgette Kubaga, ikawa ni stori bandika bandua👇

"Haya keti hapa tunataka tuzungumze na wewe kwa kujinafasi", akasema Mwenyekiti Angel Bondo kisha mazungumzo yakaendelea.....👇



Ends

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages