LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 13, 2022

SPIKA TULIA: MSIPIGE MARUFUKU USAFIRI WA MCHOMOKO+video

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson ameishauri serikali kutopiga marufuku usafiri wa taksi maarufu kama mchomoko bila kutafuta mbadala wa usafiri mwingine. Ametoa ushauri huo alipokuwa akifunga semina ya wabunge kuhusu usalama barabarani iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa jijini Dodoma Novemba 10, 2022. Semina hiyo iliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuzishirikisha taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

Mchomoko


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Vita Kawawa akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akifafanua jambo likiwemo la mabasi kuruhusiwa kusafirisha abiria hadi nyakati za usiku.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani,  Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Ramadhan Ng'anzi akielezea kuhusu sheria za usalama barabarani zinavyopaswa kutekelezwa.
Kawawa na Sagini wakisikiliza kwa makini wakati wa semina hiyo.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Fred Mwakibete akiwa makini kunukuu taarifa muhimu  katika semina hiyo.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Dkt Tulia akiishauri serikali kuopiga marufuku usafiri huo...






 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages