LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 7, 2022

RC CHALAMILA: MMOJA ALIKUWA MTUMISHI WA AIRPORT KAGERA, MWINGINE MVUVI

 Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa ufafanuzi wa idadi ya Manusura wa ajali ya Ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022 katika Ziwa Victoria mkoani Kagera, amesema idadi kamili ya Abiria walionusurika ilikuwa 24 na wawili waliofika kwenye eneo la tukio hivyo kufanya jumla ya Manusura 26.

Awali idadi hiyo ilikuwa na mkanganyiko kati ya Manusura 24 na 26 waliokuwa kwenye Ndege hiyo, hata hivyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliagiza uchunguzi wa haraka ufanyike kujua idadi kamili ya Abiria hao.

RC Chalamila amesema Mtumishi wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba alijumuishwa kwenye idadi hiyo baada ya kwenda kusaidia kwenye zoezi la uokoaji hivyo na yeye kupata mshtuko.

Manusura mwingine ni Mvuvi, aliyefahamika kwa jina la Majaliwa Jackson ambaye na yeye alikuwa kwenye zoezi hilo la usaidizi wa uokoaji baada ya Ndege hiyo kupata ajali, hivyo na yeye kupoteza fahamu wakati akiwa na harakatiza uokoaji.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages