LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 14, 2022

RAIS DK. MWINYI ATOA NENO KWA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM TAASISI YA SAYANSI ZA BAHARI, LEO

Buyu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameutaka Uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Sayansi za Bahari (IMS), Kushirikiana na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kufanya kazi ya kuielimisha jamii dhana na dhamira ya Uchumi wa Buluu kwa maendeleo ya nchi. 

Dk. Mwinyi ametoa mwito huo Buyu Mkoa Mjini Magharibi aliposhiriki katika Mahafali ya 52 Duru ya nne, ya Taasisi ya Sayansi za Bahari (IMS), Kampasi ya Buyu.

Akizungumza na Wahitimu, Viongozi wa Chuo pamoja na wananachi Mhe. Rais  Dk. Mwinyi alisema kuna umuhimu wa Uongozi wa Chuo hicho kushirikiana na Serikali na kufanya kazi ya ziada ya kuelimisha jamii juu ya dhana ya Uchumi wa Buluu na dhamira ya Serikali  ya kuweka kipaumbele katika matumizi ya rasilimali za Bahari katika kuimarisha uchumi. 

Alisema serikali itaendelea kutoa ushirikiano na IMS katika kuimarisha sekta ya Uchumi wa Buluu unaozihusisha sekta za Uvuvi pamoja na Kilimo cha Mwani kwa kuamini kuwa hiyo ndio njia bora kuibua watalamu. 

Aidha, Dk. Mwinyi alisema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Taasisi za Elimu ya Juu nchini na kubainisha uwepo wa IMS kuwa ni fursa, muhimu katika maendeleo sekta ya uchumi wa Buluu.


Alisema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa IMS katika uimarishani wa zao la Mwani, lenye kuzalisha ajira kwa kiwango kikubwa, hususani kwa akinamama. 

Alitumia fursa hiyo kuahidi kwa Uongozi wa Chuo hicho kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaijumujuisha  barabara  iendayo Chuo Kikuu katika mradi wa ujenzi wa barabara za Ndani. 

Katika hatua nyingine alitoa wito kwa wahitimu kutotosheka na Kiwango cha elimu walichofikia na badala yake kutumia taaluma na maarifa waliyonayo ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii. 
Rais wa Zanziar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi akihutubia katika Mahafali ya 52 Duru ya nne, ya Taasisi ya Sayansi za Bahari (IMS), Kampasi ya Buyu, yaliyifanyika kwenye Kampasi hiyo, Buyu Mkoa Mjini Magharibi, Zanzibar, leo.









No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages