Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameshiriki akiwa Msemaji Mkuu katika uzinduzi wa ripoti ya ufuatiliaji wa mkataba wa Nairobi, Kuhusu mkutano wa kimataifa wa idadi ya watu na maendeleo ,wenye lengo la kusimamia Utekelezaji wa makubaliano kuhusu utoaji wa huduma bora kwa akinamama na watoto,hususani masuala ya Uzazi .
Dk.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuongeza Bajeti ya Wizara ya Afya kadri hali ya Uchumi itakavyoimarika,ili kuhakikisha inatoa huduma bora za Afya nchini kote.
Amesema katika Mwaka huu wa Fedha wa 2022 Serikali imeongeza bajeti ya Wizara ya Afya kwa asilimia 8.3% kutoka asilimia 7.7.% iliotengwa katika Mwaka wa fedha wa 2019/2020,ikiwa ni juhudi za Serikali kufikia Azimio la Abuja la asilimia 15%.
Alisema ongezeko hilo la bajeti limeweza kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za Afya nyanja tofauti ,ikiwemo huduma za mama na mtoto ,huduma za watoto na vijana pamoja na uzazi wa mpango kwa jamii ya Wazanzibar kote nchini bila Malipo.
Alisema pia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ina fanyakazi kwa bidii kukomesha ukatili wa kijinsia wa aina zote,zikiwemo mimba za utotoni.
Alieleza sheria,sera na mikakati iliopo imeimarishwa ili kuakisi malengo yaliowekwa katika ngazi za kimataifa,kikanda na kitaifa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇