LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 16, 2022

DCEA YABAINI KUSHAMIRI UWEPO WA BIDHAA ZA VYAKULA VYENYE BANGI, WATOTO HATARINI KUINGIZWA KWENYE URAIBU BILA KUJIJUA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Dawa za Kuevya (DCEA) imeonya kuwa ipo hatari ya watoto kuingizwa kwenye matumizi ya dawa za kulevya bila kujua na hatimaye kuwa waraibu, kutokana na kuanza kushamiri hapa nchini tabia ya baadhi ya Wafanyabiashara kutengeneza kwa kutumia bangi bidhaa za vyakula hasa zinazopendwa na watoto.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Gerald Kusaya imetaja baadhi ya bidhaa zilizobainika kukutwa na zikiwa zimetengenezwa kwa kutumia bangi ni pipi, keki Ice Cream na biskuti biadhaa ambazo hupendwa zaidi na watoto.

Kamishna Jenerali Kusaya amesema, katika kipindi cha mwezi Oktoba na mwanzoni mwa mwezi Novemba 2022, DCEA kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na Usalama  walimata  'Biskuti' 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa za kelevya aina ya Bangi kama moja ya malighafi na jumla ya kilo 34.89 za dawa za kuevya aina ya Heroin, katika Oparesheni iliyofanywa na vyombo hivyoa katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema pamoja na kukamata 'Biskuti' hizo 50 zilizotengenezwa kwa kutumia bangi na kilo 34.89 za dawa za kulevya aina ya Heroin katika Operesheni hizo, Jijini Arusha walikamata Mtuhumiwa Hassan Ismail (25) mkazi wa  Olasiti jijini humo ambaye nayesadikiwa kuwa ndiye mtengenezaji wa biskuti hizo zenye dawa za kulevya, akiwa pia na dawa za kulevya aina ya bangi.

"Matukio ya uwepo wa bidhaa za vyakula vinavyotengenezwa kwa kutumia bangi yameanza kushamiri hapa nchini.  Itakumbukwa kuwa mwaka 2020 na 2021 Mamlaka ilikamata bangi iliyosindikwa mfano wa jam keki na asali katika matukio tofauti wakati wa utekelezaji wa operesheni zake"

Hali hii inaonesha wazi kuwa tatizo hili limeanza  kushamiri nchini na hasa ikizingatiwa kuwa wafanyabiashara hawa wenye nia ovu hutumia vyakula vinavyopendwa na watoto mfano pipi, keki Ice Cream na biskuti hivyo, kuwepo na uwezekano wa kuwaingiza watoto kwenye matumizi ya dawa za kulevya bila kujua na hatimaye kuwa waraibu. Hivyo natoa mwito kwa wazazi na walezi kufuatilia kwa ukaribu nyendo za watoto wao", alisema Kamishna Jenerali Kusaya.

Askari wakitazama Biskuti zilizotengenezwa na bangi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages