LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 13, 2022

BAADA YA MIEZI MITATU KAGERA, RC CHALAMILA AGUNDUA VIPAUMBELE VYENYE TIJA, AMPONGEZA RAIS SAMIA

Na Lydia Lugakila, Kagera.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema tangu Julai 28,2022 hadi sasa ametimiza miezi mitatu tangu ateuliwe na  Rais Samia Suluhu Hassan kuuongoza mkoa huo na kuwa baada ya kuujua  vizuri amegundua vipaumbele kadhaa vyenye tija vinavyoweza kuufanya mkoa huo kupanda juu zaidi kiuchumi huku akimpongeza Rais Samia kwa kuboresha sekta kadhaa ndani ya mkoa huo.


Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mkoa wa Kagera, RC Chalamila amesema kuwa mkoa wa Kagera wenye watu takribani  Milioni 2.9 umekuwa ukifanya vizuri katika sekta ya kilimo huku matarajio yake yakiwa ni kuliendeleza  zao la ndizi na kulifanya kuwa la kibiashara zaidi ambapo tayari maandalizi ya kutuma ujumbe wa wataalam kwenda nje ya nchi zinazolima na kusafirisha ndizi kwa wingi yameanza.


"Ndizi zetu zitaanza kutumwa kitaalam ili kumuokoa mkulima wa kawaida wa zao hilo katika dunia nchi kubwa kwa kusafirisha ndizi kwenda nchi za ulaya ni Jamaica ikifuatiwa na Brazil hivyo tujipange Kisawa sawa alisema Chalamila".


Kwa upande wa zao la kahawa  amesema kazi iliyopo kwa sasa ni kuhamasisha zaidi katika uwekezaji katika sekta ya kahawa ili kupandisha thamani ya zao hilo na kuongeza viwanda huku akiwataka wawekezaji zaidi kujitokeza ili zao hilo liwe na tija kubwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi.


Katika sekta ya elimu amempongeza Rais Samia kwa kuboresha sekta hiyo hasa kufuta ada kwa shule za msingi hadi kidato cha sita ili kuruhusu kuwepo kwa shule nyingi.


Aidha ameongeza kuwa mkoa huo umejipanga kila mwaka kufuatilia wanufaika wa bodi ya mikopo wanufaika wa elimu ya juu, ambapo watatakiwa kujua ni wanafunzi wangapi wanufaike kila mwaka hivyo ofisi yake kwa kushirikiana na wabunge lazima wahakikishe wanapambana na suala hilo ambapo tayari Rais Samia ameisha wekeza zaidi Bilioni 400 ili kuhakikisha fedha hizo zinalipa ada ya wanafunzi elimu ya juu.


Hata hivyo katika sekta ya mifugo na uvuvi mkuu huyo wa mkoa amesema watapitia upya lanchi na ikigundulika kuna ufugaji wa kawaida usio na tija mkataba utasitishwa kwa haraka ili kuruhusu wawekezaji wenye kuwekeza kiukweli ukweli waanze kazi hiyo ambapo pia ameongeza kuwa uwepo wa ziwa Victoria ni fursa ya kiuchumi na kuwa Rais Samia amekubali wavuvi waanze kupata mikopo isiyo na riba kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya uvuvi


RC Albert Chalamila

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages