Na CCM Blog
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye aliwasili jana Seoul Korea Kusini, leo anatarajiwa kutembelea Kampuni ya kutengeneza mabehewa na injini za treni cha SRT kilichopo katika mji wa viwanda wa Mungyeong na kituo cha ubunifu kilichopo Pangyo.
Aidha, akiwa Korea Kusini, Waziri Mkuu anatarajiwa kushiriki Kongamano la Biashara na kukutana na wamiliki wa Kampuni kubwa na wenye viwanda na pia atakutana na Watanzania waishio Korea Kusini.
Kupitia vikao hivyo, Tanzania inatarajiwa kuimarisha mahusiano na Korea Kusini ambayo yamedumu kwa miaka 30. Vilevile, itatoa fursa ya kukuza mahusiano ya kibiashara na uwekezaji, kuangalia fursa za kukuza uchumi wa bluu, utalii, mahusiano ya anga na ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na utamaduni.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇