Wataalamu wa upasuaji moyo na mishipa ya damu kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimfanyia upasuaji wa kutengeneza valvu ya upande wa kushoto wa moyo mtoto ambaye valvu yake ilikuwa inavuja damu. Upasuaji huo umefanyika katika kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyoanza leo JKCI ambapo watoto 60 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua.
Madaktari bingwa wa usingizi na wagonjwa mahututi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao kutoka Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakihakikisha Valvu iliyofanyiwa marekebisho inafanya kazi vizuri kwa kutumia mashine ya Trans esophageal ECHO kabla ya kutoa moyo katika mashine ya kuusaidia moyo na mapafu kufanya kazi wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyoanza leo katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa kuendesha mashine ya kuusaidia moyo na mapafu kufanya kazi (Heart Lung Machine) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzake kutoka Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakichukua taarifa za mgonjwa anayefanyiwa upasuaji wa moyo kutoka kwenye mashine hiyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo kwa watoto iliyoanza leo JKCI ambapo watoto 60 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua.
Picha Khamisi Mussa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇