Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma, Oktoba 29, 2022, kuhusu utekelezaji wa majukumu yao na vipaumbele kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mativila pamoja na mambo mengine alielezea kuhusu mtandao wa barabara wanazozisimamia nchini kuwa hadi sasa zimejengwa zaidi ya kilomita 11000 za lami.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Zamaradi Kawawa akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS, Mhandisi Boniface Mkumbo akielezea hatua ambayo ujenzi wa barabara ya Ringroad mkoani Dodoma ilipofikia.
Afisa Habari Mwandamizi wa TANROADS, Lela Muhaji na Zamaradi Kawawa wakiandika mambo muhimu wakati wa mkutano huo.Wanahabari wakiwa makini na kazi yao.
Mwandishi wa Habari wa EATV, Daniel Mkate akiuliza swali.
Mwandishi wa habari na mmiliki wa Kamanda wa Matukio Online TV, Kamanda Richard Mwaikenda akiuliza swali kwamba TANROADS ina mpango gani wa kupunguza matuta katika barabara ya Tunduma- Sumbawanga?
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mhandisi Mativila akielezea zaidi...IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇