Taa mpya zilizowekwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) maeneo ya Mjimwema, Stendi ya zamani na Ubena katika Mji wa Njombe zimesababisha mkanganyiko mkubwa kwa watembea kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto wasiojua matumizi ya taa hizo.
Mwandishi wa habari hii, Richard Mwaikenda alishuhudia mkanganyiko huo katika taa zilizopo stendi ya zamani ambapo alichukua baadhi ya matukio kuonesha hali halisi pamoja na kuhojiana na baadhi ya wananchi walio karibu na taa hizo pamoja na baadhi ya wananchi waliokuwa wanavuka eneo hilo kwa kudra za Mwenyezi Mungu.
Watembea kwa miguu wakivuka barabara licha ya taa kuonesha nyekundu katika eneo la stendi ya zamani mjini Njombe septemba 30, 2022.
Mtembea kwa miguu akihatarisha maisha yake kwa kuvuka wakati taa imewaka nyekundu kumkataza na kuruhusu magari.
Kijana akivuka licha taa kuonesha alama nyekundu.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kuona/kusikiliza kupitia clip hii ya video, kuhusu mganganyiko uliotokea katika taa zilizowekwa karibu na stendi ya zamani ya mjini Njombe pamoja na maoni yaliyotolewa na wananchi hasa kuhusu umuhimu wa kutolewa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya taa hizo....
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇