Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania, Dkt Stella Bitanyi amesema kuwa nyama ya nguruwe maarufu kama Kitimoto ni salama kama ilivyo kwa nyma za wanyama wengine, ila kichotakiwa ni kuzingatia usafi wakati wa ufugaji na uaandaaji wa nyama. Amebainisha hayo alipokuwa ajibu swali kuhusu madhara ya nyama hiyo wakati wa mkutano na vyombo vya habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dodoma Oktoba 21, 2022 ambapo pamoja na jambo hilo alizungumzia utendaji wa taasisi hiyo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa akihitimisha mkutano kati ya wanahabari na Wakala hiyo.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano huo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Dkt akielezea kuhusu nyama hiyo ya nguruwe...IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇