Na Christopher Lissa, Songwe
Kampuni ya Kenya ya utengenezaji na usambazaji wa mbolea ya SBL, imeahidi kutoa zawadi ya mfuko mmoja kwa kila mkulima atakayetembela Banda la Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na kununua mifuko kuanzia mitatu ya mbolea ya SBL, katika Maonyesho ya Siku ya Mbolea Duniani yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Kimondo, mkoani Songwe.
Ahadi ya neema hiyo kwa wakulima nchini imesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Joe Kariuki, wakati akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Maonyesho hayo jana na kuongeza kuwa hiyo ni sehemu ya SBL kuunga mkono jitihada za Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kumwinua mkulima Nchini.
"SBL imeonyesha ufanisi mkubwa nchini Kenya. Sasa tunataka hata hapa Tanzania wakulima wanufaike nayo na kwa kuanzia tunatoa mfuko mmoja wa kilo 25 bure kwa wateja watakaofika katika maonyesho haya hapa Songwe,"alisema Joe na kuongeza kwamba SBL kupitia TFC imeingiza nchini mifuko 2,500 ya mbolea hiyo ya 'Organic' ambayoni rafiki wa mazingira.
"Mifuko hiyo 2,500 ilmeingia Songwe na tutauza na baadhi kuigawa bure hivo Wananchi waje katika Uwanja wa Kimondo, Mlowo na wafike katika Banda la TFC" ameongezs Joe.
Awali Kaimu Meneja wa Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC Kanjel Mloba alisema mbolea hiyo ya SBL imeingizwa nchini kutokana na ubora wake na ufanisi iliounyesha huko Kenya.
"Pamoja na mbolea nyingine leo (jana) katika Maonyesho haya TFC tumetambulisha mbolea hii ya SBL ambayo ni organic, ni mbolea nzuri na tunahimiza wakulima kuitumia", alisema Kanjel na kuongeza kuwa TFC itaendelea kuhakikisha inawasaidia wakulima kuwafikishia mbolea bora ili kilimo chao kiwe chenye tija.
Maonyesho hayo ya Siku tatu yaliyoanza jana kwa kuandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania TFC yanatarajiwa kufungwa na Wazirii wa Kilimo Hussein Bashe kesho Oktoba 13 mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Utengenezaji Mbolea ya SBL ya Kenya Joe Kariuki akizungumzia na waandishi wa habari Katika Viwanja vya Kimondo, Mlowo, Mbozi mkoani Songwe. (Picha na Christopher Lissa).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇