Na Christpher Lissa, Mbozi Songwe
Baada ya Kampuni ya SBL inayozalisha mbolea ya GPC kutoka Kenya kuahidi kugawa bure mifuko 2,500 ya mbolea kwa wakulima watakaofika kwenye Maonyesho ya Mbolea yanayoanza leo Kitaifa katika Viwanja vya Kimondo Mloo Mbozi mkoani Songwe, sasa SBL watakabidhi bure mbolea hiyo kwa Mamlaka ya Mbolea (TFC).
Awali Mkurugenzi wa Kampuni ya SBL Joe Kairuki alisema Kampuni hiyo ilitarajia kugawa bure mifuko hiyo 2,500 ya mbolea kwa wakulima watakao fika kwenye Maonyesho hayo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwainua wakulima nchini.
Kairuki alisema, mbolea ya GPC imefanya vizuri nchini Kenya na anaamini italeta tija kubwa kwa wakulima hapa Tanzania na kuwasihi wakulima kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho ili kujua namna mbolea hiyo ilivyo bora.
Your Ad Spot
Oct 11, 2022
Home
Biashara
featured
SBL KUKABIDHI TFC MIFUKO 2,500 YA MBOLEA BADALA YA WAKULIMA KWENYE MAONYESHO YA MBOLEA YANAYOANZA KITAIFA LEO SONGWE
SBL KUKABIDHI TFC MIFUKO 2,500 YA MBOLEA BADALA YA WAKULIMA KWENYE MAONYESHO YA MBOLEA YANAYOANZA KITAIFA LEO SONGWE
Tags
Biashara#
featured#
Share This
About Bashir Nkoromo
featured
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇