LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 21, 2022

RAIS SAMIA APOKEA RIPOTI YA KIKOSI KAZI KUHUSU URATIBU MAONI YA WADAU WA DEMOKRASINA YA VYAMA VINGI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

Dar es Salaam, leo

Rais Samia Suluhu Hassan amepokea Ripoti ya Kikosi Kazi kuhusu Uratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa katika hafla iliyofanyika  Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.

Akikabidhi Ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Profesa Rwekaza Mukandala  amesoma Mapendekezo 18 yafuatayo;

1. Kikosi kazi kinapendekeza mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa katiba na sheria, mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote, yafanyike marekebisho ya sheria ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi.

2. Sheria ya vyama vya siasa ifanyiwe marekebisho ili kulipatia baraza la vyama vya siasa linaloundwa na vyama vyenyewe mamkala ya kushughulikia swala la uvunjifu wa maadili ya vyama vya siasa kupitia kamati yake ya maadili, msajili wa vyama vya siasa aandae muongozo wa chaguzi za ndani za vyama vya siasa.

3. Mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku kwa vyama vya siasa uendelee, isipokuwa 10% ya fedha zinazotolewa sasa zitolewe kwa mgawanyo sawa kwa vyama vyote vyenye usajili kamili.

4.Tume ya taifa ya Uchaguzi isilazimike kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, chama chochote cha siasa, taasisi au asasi yoyote na utendaji wake uruhusiwe kuhojiwa kwenye mahakama ya juu ili kuongeza uwajibikaji wa tume.

5. Wajumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi wateuliwe na kamati inayoongozwa na jaji mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mwenyekiti) jaji mkuu wa Zanzibar (M/mwenyekiti), kamishna wa serkretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Tanzania bara, mwenyekiti wa tume ya maadili ya viongozi wa umma ya Zbar, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na wajumbe 2 watakaoteuliwa na jaji mkuu wa JMT baada ya kupendekezwa na chama cha wanasheria Tanganyika na chama cha wanasheria Zbar. Pia, angalau wajumbe wawili wa uteuzi wawe wanawake, sifa za kuwa mwenyekiti, makamu au mjumbe ziainishwe, nafasi za ujumbe zitangazwe, watu wafanyiwe usaili kisha majina yapelekwe kwa Rais kwa uteuzi

6. Matokeo ya Uchaguzi wa Rais jahojiwe kwenye Mahakama ya juu

7. Wasimamizi wa uchaguzi wazingatie sheria, maadili, weledi, uwazi na ushirikishwaji wa wadau wakati wa kufanya kazi zao. Wasimamizi watakaokiuka taratibu wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.

8. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ipewe fedha kwa wakati

9. Itungwe sheria kusimania shughuli za tume ya uchaguzi, pia iwepo sheria moja ya kusimamia chaguzi zote, maafisa wa uchaguzi wanaoengua wagombea bila sababu maalumu wawajibishwe

10. Matumizi ya tehama kwenye uchaguzi yaboreshwe

11. Sharti ya uwepo wa sera ya jinsia liwepo kwenye sheria za vyama vya siasa, pia ushiriki wa wanawake kwenye vyombo vya maamuzi isipungue 40%

12. Sheria zinazokwamisha ushiriki wa wa watu wenye ulemavu kwenye siasa ziangaliwe upya

13. Juhudi za ushirikishwaji wa vijana kwenye siasa ziongezwe

14. Serikali iongeze utoaji wa elimu ya uraia, pia ifundishwe kwenye ngazi zote za elimu, pia mtaala wa elimu uzingatoe elimu ya uraia.

15. Swala la rushwa litamkwe katika katiba ya nchi ili wananchi waelewe

16. Kuanzishwe utaratibu wa mijadaa kila mwaka itakayohusisha viongozi wakubwa wa kitaifa na kisiasa ili kudumisha mshikamano, mahakama iwe ni mamlaka ya mwisho ya kuamua pindi maridhiano yanapokwama

17. Wanahabari waunde chombo cha kusimamia wanahabari na vyombo vyao, vyombo vya umma vitoe muda sawa wa kutangaza habari za wagombea wa vyama vyote kwa usawa, uwepo mchakato wa wazi wa kuwajibisha vyombo vya habari badala ya kufungiwa pekee na mkurugenzi wa habari na mawasiliano

18. Mchakato wa katiba mpya uendelee, hata hivyo mjadala wa kitaifa kuhusu katiba mpya uanze kabla ya kuanza kwa mchakato wa kuandika katiba mpya ili kujadili ajenda muhimu za muungano, mamlaka ya Rais, Rushwa, tume ya uchaguzi n.k

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Profesa Rwekaza Mukandala katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 21, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Profesa Rwekaza Mukandala katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 21, 2022. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Hamad Rashid Mohamed.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa Profesa Rwekaza Mukandala pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho Hamad Rashid Mohamed, baada ya kupokea Ripoti ya Kikosi Kazi hicho, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 21, 2022. (PICHA NA IKULU)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages