Na Bashir Nkoromo, CCM Blog.
Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza lake la Mwaziri, akimteua aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Stergomena Taxi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kuchukua nafasi ya aliyekuwa anashika nafasi hiyo Balozi Liberata Mulamula.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu Jijini Dar es Salaam, Oktoba 2, 2022 usiku, imesema katika mabadiliko hayo, pia Rais amemteua aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Ras amemteua pia Angella Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati huohuo kumteua kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
"Mawaziri walioteuliwa Wataapishwa leo Oktoba 3, 2022, Ikulu Jijini Dar es Salaam", Taarifa hiyo imesema.
Your Ad Spot
Oct 3, 2022
Home
featured
Kitaifa
RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI, ALIOWATEUA KUWAAPISHA LEO OKTOBA 3, 2022
RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI, ALIOWATEUA KUWAAPISHA LEO OKTOBA 3, 2022
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About Bashir Nkoromo
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇