LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 22, 2022

NFRA: TUNA AKIBA YA KUTOSHA YA CHAKULA CHANYE UBORA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), CPA Milton Lupa ameuthibitishia umma kuwa wanayo akiba ya kutosha ya chakula tena chenye ubora. Amebainisha hilo baada ya Mwandishi wa Blog ya Taifa ya CCM (CCM BLOG) na Kamanda wa Matukio Online TV, Richard Mwaikenda kuuliza swali kwamba wakala ina mkakati gani wa kuhakikisha inakuwa na chakula cha kutosha ili kupunguza upungufu wa chakula unaosababisha hivi sasa bei ya mazao kupanda. Pamoja na mambo mengine, CPA Lupa ametoa uhakika huo wakati wa mkutano na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, jijini Dodoma Oktoba 22, 2022, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo.



Mkurugenzi wa Hifadhi ya Chakula NFRA, Dkt Silivano Mwakinyali akielezea madhara ya sumu kuvu kwenye mazao.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa akihitimisha mkutano huo.
 

Wanahabari wakisikiliza kwa makini wakati CPA Lupa akifafanua mambo. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, CPA Lupa akielezea kuhusu akiba ya chakula kilichopo....IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages