Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deo Ndejembi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia Mpango wa Urasimishaji Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) zaidi ya sh. bilioni 4 kwa ajili ya urasimishaji ardhi, mashamba na biashara za wanyonge nchini.MKURABITA ipo chini ya ofisi hiyo.
Shukrani hizo amezitoa kwa nyakati tofauti wakati wa uzinduzi wa majengo ya masijala katika vijiji vya Mbondo na Nakalonji wilayani Nachingwea, Lindi Oktoba 12, 2022.
Ndejembi na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu Masyenene na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea wakiwa na furaha baada ya uzinduzi wa masijala hiyo.Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Mujungu Masyenene akiwasalimia wananchi.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo.
Naibu Waziri Ndejembi akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Ndejembi pamoja na mambo mengine akitoa shukrani hizo kwa Rais Samia.....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇