LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 22, 2022

NAIBU KATIBU MKUU MPANJU: HAMASISHENI WATANZANIA WASHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO+video

 

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Amon Mpanju amewataka viongozi wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini kutumia ujuzi na uzoefu walionao  kwenda kuzalisha wataalamu wenye ueledi, waadilifu, wazalendo walio tayari kwenda kuwahudumia watanzania maeneo wanakotoka.

 Mpanju amebainisha hayo wakati wa kufunga mafunzo ya kikosi kazi cha viongozi hao, jijini Dodoma leo, yenye lengo la Kufanya tathmini ya  namna walivyotekeleza majukumu yao ya vyuo kwa mwaka 2021/ 2022 na kubainisha changamoto pamoja na kujiwekea mikakati ya namna ya kuzitatua.

Aidha, Mpanju amesema kuwa nia ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona sekta ya maendeleo ya jamii inakwenda kuamsha ari, kuhamasisha watanzania  kufungua akili na uelewa  ili washiriki katika shughuli za maendeleo katika ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.

 Naye Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, Neema Ndoboka alisema kuwa kabla ya kuanza mafunzo washiriki walikumbushwa kuhusu Nidhamu kazini, fedha, ukaguzi, mipango na bajeti,mikataba na matumizi ya sahihi ya tehama.

Neema akiteta jambo na Naibu Waziri Mpanju.
Neema akiongoza mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo








 Naibu Waziri Mpanju akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mpanju akitoa agizo hilo...

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages