Na Jacquelin Liana, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kanali Mstaafu Komredi Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa Makamu Mwenyekiti wa TCD Mwenyekiti wa Chama cha Civic United Front (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, wameongezewa muda wa kuendelea kukiongoza kituo hicho.
Hilo limejiri, baada ya Viongozi Wakuu wa Vyama Wanachama wa Kituo hicho (TCD), kwa kauli moja kupitisha azimio la kuwaongezea muda wa kuongoza kituo hicho, katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam, jana Oktoba 24, 2022.
Katika kikao chao cha Oktoba 24, 2022, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, viongozi hao wakuu wa vyama walipitisha azimio hilo kwamba Komredi Kinana na Prof Lipumba wataendelea na uongozi wa TCD hadi Juni 30, 2023.
Pamoja na CCM na CUF, vyama vingine wanachama wa TCD ni NCCR-Mageuzi, ACT-Wazalendo, CHADEMA na CCK.
Your Ad Spot
Oct 25, 2022
KINANA, LIPUMBA KUENDELEA KUIONGOZA TCD
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇