Mwenyekiti wa UWT Dar es Salaam Florence Masunga, amewapa shime wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Keko Magurumbasi akiwahamasisha kuhakikisha kesho Jumatano, Oktoba 5, 2022, wanafanya mitihani yao vema ili wafaulu wote kama moja ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazofanya katika kuinua sekta ya elimu nchini.
Masunga alitoa shime hiyo, alipotembelea jana shule hiyo kuwapa vifaa vya kufanyia mitihani na kuwafunda namna bora ya kufanya mitihani, ambapo aliwataka wasiihofie mitihani wajisikie kama wanaofanya mitihani ya kawaida ambyo hupewa na walimu wao darasani mara kwa mara.
"Kwanza mtakapoingia darasani kila mmoja amuombe kwanza Mungu, kisha awe mtuivu, msimuogope msimamizi, pale utakapoona kuna jambo linakukwaza nyoosha mkono kumwita msimamizi kwa nidhamu kisha muombe akusaidie.
Kumbukeni Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada kubwa katika kuboresha elimu hapa nchini, sasa mkifanya mitihani vizuri na kufaulu ndiyo itakuwa moja ya kuunga mkono juhudi hizi za Rais Samia", akasema Mama Masunga.
Tafadhali, msikilize hapo👇
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇