LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 6, 2022

DC DODOMA AIPONGEZA MKURABITA KUANZISHA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO SOKO LA MACHINGA DODOMA+video

 

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya mpango wa urasimishaji na uendelezaji  biashara kwa wafanyabiashara wa Soko jipya la Machinga Dodoma Jiji, yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) katika ukumbi uliopo katika soko hilo Oktoba 6, 2022.

DC Shekimweri ameupongeza uongozi wa MKURABITA wa kuendesha mafunzo hayo na kutoa wito kwa taasisi na wadau kushirikiana kuwaendeleza wamachinga.

Aidha, DC Shekimweri amewataka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuiga mfano wa MKURABITA kwa kutoa elimu kwa wamachinga kabla ya kuanza kuwatoza kodi kwa nguvu.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa MKURABITA, Dkt, Seraphia Mgembe alielezea lengo la kuendesha mafunzo hayo kuwa ni: kuwajengea uwezo wa kiuchumi wamachinga,  uanzishwaji wa vituo jumuishi vya urasimishaji na uendelezaji biashara, kuunganishwa  kwa wadau na uwezeshwaji wa mitaji.

Taasisi zilizoshiriki katika mafunzo hayo ni:Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara,  Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Jeshi la Polisi Jamii, Shirikisho la Umoja wa Machinga Mkoa wa Dodoma na Taasisi za Fedha.


Mkurugenzi Mtendaji wa MKURABITA, Dkt, Seraphia Mgembe akielezea lengo la kuendesha mafunzo hayo kuwa ni: kuwajengea uwezo wa kiuchumi wamachinga,  uanzishwaji wa vituo jumuishi vya urasimishaji na uendelezaji biashara, kuunganishwa  kwa wadau na uwezeshwaji wa mitaji.

Mwenyekiti Msaidizi wa Shirikisho la Machinga Mkoa wa Dodoma, Christian Msumari akitoa shukrani kwa serikali na MKURABITA kwa kuwajali wamachinga.

Afisa wa Jeshi la Polisi Ushirikishwaji  Wilaya ya Dodoma, ASP Keneth Muhanga  akielezea jinsi ulinzi utakavyokuwa katika soko hilo la Machinga.
Meneja wa Tawi la NMB  Benk,  Amos Mubusi akielezea jinsi benki hiyo itakavyokuwa karibu na wamachinga katika soko hilo ikiwemo kuwapatia mikopo. 

Baadhi ya wadau na viongozi wa  Machinga wakihudhuria mafunzo hayo.

Afisa Urasimishaji na Uendelezaji Biashara wa MKURABITAZabron Makoye akiendesha mafunzo hayo
 
Sehemu ya muonekano wa soko jipya la Machinga Dodoma.





Mgeni rasmi, DC Shekimweri akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa MKURABITA.
DC Shekimweri na Dkt Mgembe wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria mafunzo hayo.
                      
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITAMujungu Kasyenene akimsindika DC Shekimweri  baada ya mafunzo kuzinduliwa.




DC Shekimweri akiagana na Dkt Mgembe.



DC Shekimweri akiagana na Mwenyekiti Msaidizi wa Machinga Mkoa wa Dodoma, Msumari.



PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, DC Shekimweri akizindua mafunzo hayo, Dkt Mgembe akielezea lengo la mafunzo hayo na Mmachinga Msumari akitoa shukrani pamoja na Mkurugenzi wa Fedha MKURABITA, Kasyenene akitoa shukrani kwa mgeni rasmi...



IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages