Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amekemea tabia ya utoaji na upokeaji rushwa, kuzushiana uongo, hila na kuchafuana kisiasa katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu wa Chama unaoendelea katika ngazi mbalimbali nchini.
Katibu Mkuu ameeleza kuwa, Chama kinaendelea kufuatilia kwa karibu wale wote wanaotoa na kupokea rushwa na hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa kwa mujibu wa katiba, sheria na Kanuni za Chama.
Amewaasa wagombea wote wazungumze sifa na mazuri yao na nini wanatarajia kuwafanyia wanachama na wananchi kwa ujumla pindi watakapochaguliwa na sio kuwachafua na kuwatengenezea ajali wagombea wengine, kwani Chama kikibaini hayo kitachukua hatua kwa mujibu wa utaratibu, ikiwemo kuwaondoa katika orodha ya wagombea.
Katibu Mkuu Ndugu Chongolo ameyasema hayo hivi karibuni katika Kongamano la mafunzo ya Uongozi, Itikadi na Uzalendo Mkoa wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇